TEF YATANGAZA MAKONDA ADUI WA UHURU WA HABARI
Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) leo limevitaka vyombo vya habari nchini kutokuandika au kutangaza habari zozote zinazomhusisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
TEF wameyasema hayo leo katika taarifa yao na kulaani vikali kitendo cha Makonda cha kuvamia kituo cha Utangazaji cha Clouds usiku wa Machi 17 akiwa na askari wenye silaha.
“Kwa mantiki hiyo, tunamtangaza Ndugu Paul Makonda kuwa ni Adui wa Uhuru wa Habari, na yeyote yule atakayeshirikiana naye katika kukandamiza uhuru wa habari nchini,” ilisema taarifa hiyo ya TEF iliyoandikwa na Mwenyekiti wake, Theophil Makunga.
Post a Comment