Header Ads

CHADEMA Watangaza Mgogoro Na RC Makonda


Ndugu viongozi Wabunge,Mameya,Madiwani,Wenyeviti wa Serikali za Mitaa pamoja na viongozi na Wanachama wa Chama Mkoa wa Dar Es salaam naomba kwa niamba ya Baraza maalum la Kanda ya Pwani ambalo lilikuwa likihutubiwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe.Freeman Mbowe kwa kauli Moja wajumbe wote wameridhia kutokushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es salaam Bwana Makonda kutokana na shutuma mbalimbali alizonazo.

Nikiwa kama kama Katibu wa Chadema Jiji hili naunga Mkono kutomtambua Bwana Paul Makondi mpaka hapo atakapo tolea ufafanuzi tuhuma zake... moja ya tuhuma zake, Ni Vyeti Vyake Vya Elimu,Kuwa na Mali ambazo zinawalaki,kuhusishwa kuvamia kituo kimoja cha TV na Radio.... Tuhuma hizi mpaka sasa hazijatolewa ufafanuzi.

Mkumbuke ya kwamba Jiji hili la Dar Es salaam lipo chini ya Ukawa... Ni mwiko na marufuku kwa Diwani yeyote ama Meya au Mwenyekiti wowote Yule wa Mtaa Kuumpa ushirikiano Bwana Makonda Mpaka hapo mtakapo Arifiwa vinginevyo na Chama Mkoa Huu wa Dar Es salaam ...

By Henry Kilewo
Katibu Greater DSM

19/03/2017

Hakuna maoni