WATU 15 WAKAMATWA KWA KUKAIDI AGIZO LA SERIKALI LA LUAMS MABONDENI
Akizungumza na ITV kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Saimon Sirro amesema watu hao wamekamatwa na kupelekwa mahakamani kujibu mashtaka ya kukaidi kuhama maeneo hatarishi na kwamba eneo hilo ni mali ya halmashauri ya manispaa ya Ilala.
Hata hivyo kamanda Sirro amesema hali ya usalama katika jiji la Dar es Salaam imetengamaa, ambapo jeshi hilo limefanikiwa kudhibiti vikundi vya kihalifu.
Aidha jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata wezi wa magari na uchunguzi bado unaendelea.
Post a Comment