Header Ads

MKURUGENZI WA MAWASILIANO YA RAISI AKANUSHA HABARI INAYOSAMBAZWA KUMHUSU RAIS MAGUFULI


Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa amekanusha taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya watu kwa madai kuwa imetoka katika Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Msigwa amesema kuwa habari hiyo inayodai kuwa baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii watachunguzwa juu ya namna wanavyotumia mitandao hiyo, imetengenezwa na wahalifu wa mitandao hivyo watanzania waipuuze.

Hakuna maoni