Treni iliyopata ajali Pwani yaendelea na safari
Treni ya Deluxe Coach iliyopata ajali Jumapili hii, imeendelea na safari zake (Jumatatu) saa 9 alasiri kuelekea Kigoma na Mwanza baada ya mabahewa yaliyokuwa yamesalia kwenye reli kuondolewa.
Kwa mujibu wa Kamanda wa kikosi cha Polisi Reli, Simon Chillery, safari zimeanza baada ya kikosi cha mafundi kifanikiwa kuondoa mabehewa yaliyosalia katika reli, kati ya vituo vya Ruvu na Ngeta.
Kamanda Chillery alisema, “Treni imeondoka leo saa 9 alasiri na inatarajiwa kufika Kigoma Jumatano saa 4 asubuhi, pamoja na bado uchunguzi unaendelea kujua chanzo cha ajali, ukikamilika tutawapa taarifa
Post a Comment