Header Ads

Hii ndio kazi ambayo atakuwa ikifanya Steven Gerrard ndani ya Liverpool



Mchezaji wa zamani klabu ya Liverpool, Steven Gerrard anarudi kwenye klabu hiyo sasa atakuwa akifanya kazi kwenye kituo cha kulelea yosso klabuni hapo.

Steven Gerrard ameshafanya mazungumzo na uongozi wa klabu ya Liverpool tangu alipotangaza kustaafu kabumbu kule nchini Marekani. Amesema kwamba anajisikia vyema sana kwa kupata nafasi hiyo ya kufanya kazi kule alipoanzia kandanda lake.

Imewekwa wazi kwamba ataanza kibarua chake kipya mwezi ujao wa Februari. Pia Gerrard atafanya kazi akiwa chini ya Alex Inglethorpe kwenye kusimamia yosso wa klabu hiyo.

Hakuna maoni