AUAWA BAADA YA KUFUMANIWA AKIHONDOMOLA TENDO LA NDOA NA MKE WA MTU
WATU watatu wilayani Igunga mkoani Tabora wamekufa akiwemo mwanaume aliyeuawa na kundi la wananchi baada ya kufumaniwa akifanya mapenzi na mke wa mtu. Watoto wawili wa familia moja wamepoteza maisha kwa kuzama kwenye shimo la maji.
Akizungumza juzi mjini Tabora, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Kamishna Msaidizi Hamisi Selemani amesema katika tukio la Januari 28, mwaka huu katika Mtaa wa Stoo, Kata ya Igunga Mjini, mkazi wa Mtaa wa Masanga, Khalid Kassim (50) aliuawa na kundi la wananchi zaidi ya 100 ikidaiwa alifumaniwa akifanya mapenzi na mke wa mtu.
Kamanda Selemani amefafanua kuwa Kassim alifumaniwa na mwenye mke, Muungano Isaack (44) mkazi wa Mtaa wa Stoo.
Amesema baada ya kumfumania, Isaack alipiga kelele kuomba msaada, ndipo wananchi walitoka kwa wingi na kumshambulia kwa kipigo Kassim.
Amebainisha kuwa polisi walipata taarifa na kufika katika mtaa huo na kukuta wananchi wakiwa wamekimbia, hivyo askari walimchukua mtuhumiwa na kumpeleka Hospitali ya Wilaya ya Igunga ambako aliaga dunia wakati akipatiwa matibabu.
Kamanda Selemani amesema katika tukio la pili lilitokea siku hiyo, katika Kijiji cha Mwazizi Kata ya Bukoko, watoto wawili wa familia moja, Gumba Ngasa (2) na Kija Ngasa (1) wote wa kike, walizama maji na kufariki dunia wakati wakivuka maji.
Kamanda amesema watu wawili, Muungano Isaack na Maria Joseph wanashikiliwa na Polisi huku wengine walioshiriki mauaji ya Kassim wanaendelea kutafutwa na jeshi hilo.
Ametoa mwito kwa wazazi kuwa makini na kipindi cha masika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Dk Godfrey Mgongo amesema uchunguzi wa awali unaonesha kifo cha Kassim kilisababishwa na kuvuja damu nyingi kichwani kutokana na majeraha aliyokuwa nayo.
Aidha, Dk Mgongo alibainisha kuwa vifo vya watoto wawili Gumba na Kija vilisababishwa na maji mengi waliyomeza baada ya kuzama
Post a Comment