RADI YAUA MTU MMOJA NA KUJERUHI WANNE MBEYA
1Mtu mmoja amekufa na wengine wanne
kujeruhiwa mjini Tukuyu wilayani hapa, baada ya radi kuupiga mti
uliokuwa karibu na banda walipojihifadhi wakati mvua ikinyesha.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita karibu na vituo viwili
vya mabasi ya daladala na yaendayo mikoani kandokando ya Barabara ya
Mbeya-Malawi.
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Chalya Nyangidu alisema tukio hilo lilitokea
juzi saa saba mchana na kwamba aliyefariki dunia ni mkazi wa jijini
Arusha, Freeman Swai (35) ambaye alifika mkoani hapa kununua ndizi.
Waliojeruhiwa na kupelekwa Hospitali ya Makandana ni Oliva Ipyana (45),
Anna Jericho (30), Juliana Francis (32) na Stela Nsile (37) wakazi wa
wilayani hapa.
Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk Marco Mbata alithibitisha kupokea mwili
wa Swai na majeruhi wanne. Alisema baada ya uchunguzi ilibainika, Swai
aliungua kwa moto wa radi na kusaidiana na simu iliyokuwa ikitumia
kupiga muziki.
Post a Comment