Header Ads

Uingereza huenda ikakosa fainali za kombe la dunia 2018



Chama cha soka duniani FIFA kinakataza Serikali kuingilia masuala ya soka na adhabu kali hutolewa kwa mwanachama yeyote anayekiuka jambo hilo. Bunge la Uingereza linataka kupiga kura ya kutokuwa na imani na chama cha soka cha nchini humo FA.

Hofu imeanza kutanda kwa mashabiki wa soka nchini humo jambo hili linaweza kuwatoa Uingereza katika michuano ijayo ya kombe la dunia nchini Russia ,Endapo bunge litapiga kura wiki ijayo basi itaiweka Uingereza katika hali ya sintofahamu juu ya ushiriki wao katika kombe la dunia la mwaka 2018.
Mgogoro kati ya bunge la Uingereza na FA unakuja baada ya baadhi ya viongozi wa zamani wa FA kudai kwamba chama hicho kinashindwa kujiendesha.Katika barua ambayo viongozinwa zamani wa FA walimuandikia mwenyekiti wa kamati ya michezo bungeni bwana Damians Collin inaelezwa kwamba FA imekwama na imeshindwa kujiendesha.Inasubiriwa kwa hamu kuona nini kitatokea baada ya kikao cha bunge la Uingereza kutoa maamuzi yao kuhusu FA.
Kesi hii ya Uingereza haina utofauti na kesi iliyokuwa ikiwakabili Kuwait katika hatua ya kushiriki kombe la dunia 2018.Serikali ya Kuwait iliingilia masuala ya soka nchini humo.Wakiwa wamefika raundi ya tatu ya mechi za kufuzu kombe la dunia FIFA waliamua kuwatoa Kuwait katika mashindano hayo baada ya serikali yao kukiuka sheria za Fifa.
Uingereza ambao hadi sasa wako katika nafasi nzuri ya kufuzu kombe la dunia kwani wanaongoza kundi lao la F. Uingereza wamebakiza mechi 6 tu kufuzu kombe la dunia lakini sheria za FIFA zinaweza kuwazuia kufuzu ama kuendelea na mechi zao kwa sasa.

Hakuna maoni