Header Ads

Abdu Kiba awaonya Diamond na Alikiba ‘kuna madogo wamejipanga kuchukua nafasi zenu’ (Video)



Abdu Kiba anaamini kuwa, pamoja na kwamba kaka yake Alikiba na hasimu wake Diamond Platnumz wanaonekana kuwa juu zaidi kimuziki Tanzania, utemi wao si wa milele.
Kwenye teaser ya kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz cha Salama Jabir kitakachoruka leo saa 3 usiku kupitia EATV, Abdu amewakumbusha mastaa hao kuwa nyuma yao kuna vijana wenye hasira wanaozitafuta nafasi zao.
“[Alikiba na Diamond] waamini kuwa wapo watu wamejipanga kwaajili ya kuweza kuwatoa kwenye nafasi zao, wapo wengi ambao wana uwezo wa kufanya hivyo, nadhani bado hawajafikia muda,” anasema Abdu.
Unakubaliana naye? Unadhani kuna siku watakuja kujitokeza wasanii watakaokuwa na nguvu sawa na Kiba na Chibu? Ukichekecha akili muda huu, ni wasanii gani waliopo sasa wanaonesha dalili za kuelekea huko?

Hakuna maoni