Header Ads

Jenerali Mabeyo aapishwa kuwa Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli amemuapisha Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance S. Mabeyo.

Zoezi la kuapishwa kwa mkuu huyo limefanyika, Jumatatu hii Ikulu jijini Dar es Salaam.
Jenerali Mabeyo aliteuliwa na Rais Magufuli Alhamisi iliyopita kushika wadhifa huo baada ya Jenerali Devis Mwamunyange aliyestaafu. Jenerali Mabeyo alikuwa Luteni Jenerali kabla ya kupandishwa cheo kuwa Jenerali.
Wakati huo huo Rais Magufuli amemuapisha Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Luteni Jenerali James Mwakibolwa ambaye amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Mabeyo.

Hakuna maoni