Kinsmen!!! BAVICHA GEITA WATOA TAMKO ZITO KUHUSU WALIOTAKA VIONGOZI WA UKAWA KUJITOA,WADAI HUO NI UHUNI TU
Baraza
la vijana la Chama cha Chadema mkoani Geita limetoa tamko juu ya
upotoshaji wa mtu mmoja anayejiita Fikiri Migiyo juu ya kuwataka
viongozi wa ngazi ya kitaifa kujitoa kwenye umoja wa katiba ya wananchi
UKAWA na kusema kuwa huo ni uhuni wa mtu mmoja ambaye hawamjui hata
kwenye chama chao.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana mwenyekiti wa Bavicha mkoa wa Geita Neema
Stivin Chozaile amekanusha vikali habari hizo na kuziita ni uzushi
mkubwa sana kwani wao kama bavicha hawajafanya mkutano na kutoa tamko
kama hilo na kusema bavicha mkoa wa Geita haina katibu bali ina
mwenyekiti tu sasahawajui huyo ametokea wapi.
Mwenyekiti
huyo ameongeza kuwa hata yeye alishangaa kuona habari hizo kwenye
vyombo vya habari na kuongeza kuwa kitendo hicho cha mtu kujitambulisha
na kujiita katibu wa Bavicha mkoa wa Geita ni kiovu na na kukiita cha
kihuni na kumtaka kama anajijua ajisalimishe ndani ya siku saba kwani
kutakuwa na uchunguzi mkubwa juu ya aliyevumisha uvumi huo.
Neema
ameendelea kusema kuwa huenda ni Mbinu za CCM na waache mara moja
kukichafua chama hicho na wao kama Bavicha mkoa wa Geita wanaiunga mkono
asilimila miamoja muungano wa vyama hivyo na kuwata wananchi wa mkoa
wa Geita kuacha kusikiliza poropaganda za watu wasiokuwa na msimamo kama
CCM.
.
Kwa
upande wa katibu wa chadema wilaya ya Geita Rogers Luhega amesema kuwa
hizo ni mbinu chafu tu za watu wanaoweweseka na UKAWA ulivyojipanga kwa
kuwakomboa wananchi kwani uchaguzi wa task force uliofanyika
hivikaribuni mjini hapa hakuna jina la kiongozi huyo iwe wilayani ama
mkoani na hatumjui kabisa sisi tunaendelea na vikao na wenzetu cuf kwa
ajili ya mapokezi ya wageni wetu jumatatu ijayo.
Naye
Abdalah Tungaraza mwanachama wa CUF ambaye pia ni Ukawa amelaani tamko
la mtu huyo ambaye hajulikani hata anwani yake wala makazi yake na
kuongeza kuwa sisi ukawa tutahakikisha hakuna mtu wakutuchonganisha kwa
lolote lile.
Uvumi huo umekuja na kuonekana kwenye vyombo mbalimbali vya habari kukiwa
ni siku chache viongozi wa ukawa kuanza ziara mkoani hapa kwa kutaka
kuwaeleza watanzania juu ya kinachoendelea juu ya mchakato wa katiba .USIKOSE KUFATILIA MATOWO BLOG KWA HABARI ZAIDI
ASANTENI SANA
ASANTENI SANA
Post a Comment